Siku
moja Jimi alimwuliza mtu mmoja anayekana kuwa kuna Mungu endapo alipata
kujaribu sana, hata kwa dakika chache tu, kupigana na wazo lisemalo
kwamba huenda Mungu yuko.
"Sawa
kabisa!" mkana Mungu yule akajibu, akimwacha Jimi na mshangao.
"Miaka mingi iliyopita, mimi nilikuwa karibu sana nigeuke na kuwa
mtu anayemwamini Mungu. Nilipokiangalia kile kiumbe kidogo sana - lakini
- kikamilifu katika kitanda chake kidogo, nilipochungulia na kuviona
vidole vile vidogo fahamu za kwanza za kutambua, nilipita katika kipindi
cha miezi kadhaa ambayo katika hiyo mimi nilikuwa karibu kabisa niache
kuwa mkana Mungu. Kule kumwangalia mtoto yule kulikuwa kumenishawishi
karibu kabisa kuwa hapana budi Mungu alikuwa yuko."
1.
Kila Kitu Kilichobuniwa Kina Mbunifu Wake
Muundo
wa mwili wa kibinadamu unafanya iwepo haja ya kuwako mbunifu wake.